Home Uncategorized HABARI NJEMA!! DUDUBAYA AOKOKA, AFANYIWA MAOMBI YA KUFA MTU

HABARI NJEMA!! DUDUBAYA AOKOKA, AFANYIWA MAOMBI YA KUFA MTU


Msanii nguli wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini, maarufu kama Dudubaya ama Konki Master, ameamua kuokoka na kumrudia Mungu, jambo ambalo liimewaacha mdomo wazi watu wengi.

Taarifa za Dudubaya kuokoka zilianza kusambaa kupitia mitandao ya kijamii, huku yeye mwenyewe akipost na kuandika; “MZIGO MZITO NIMEUTUA…….. SINA ADUI TENA…. SINA MSHINDANI TENA… BAADA YA KUSAMEHE YOTE NIMEYASAHAU…… I AM KONKI 3 MASTER”. Baada ya post hiyo pia aliweka video ikimuonyesha akiombewa na Mchungaji Boniface Mwamposya ‘Mpaka Mafuta wa Bwana’.

Naye mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, Emmanuel Mbasha, ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba:  “Nikiwa kama baba mlezi wa waimbaji wote wa nyimbo za injili Tanzania nachukua nafasi hii kukupongeza ndugu yangu Konki Master kwa uamuzi wako mzuri wa kumpokea Yesu Kristo.

“Hii ni hatua nzuri ya kuigwa na pia kupongezwa maana kwa Yesu ndiyo kuna kila kitu. Kama hauna wivu wa ki pepo naomba ushiriki kumpongeza Monki Master kwa hatua njema hii aliyochukua.”

SOMA NA HII  LUKAKU APATA TIMU MBADALA