Home Habari za michezo FT: YANGA 3-0 MADEAMA….PACOME KAMA ONANA….MUDATHIRI ‘KAZIKA MAZIMA’…..

FT: YANGA 3-0 MADEAMA….PACOME KAMA ONANA….MUDATHIRI ‘KAZIKA MAZIMA’…..

Habari za Yanga leo

IKIWA ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mkapa Yanga wamepata ushindi wa magoli  3-0 dhidi ya Medeama ya Ghana.

Ni bao la nyota Pacome Zouzoua ambaye kafunga katika kipindi cha kwanza muda mfupi kabla ya kwenda mapumziko.

Ilikuwa dakika ya 33 nyota huyo wa kazi alipachika bao hilo lililowanyanyua mashabiki wa Yanga.

Bao hilo linawapa uongozi Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi katika msako wa kutinga hatua ya robo fainali Afrika.

Kipindi cha pili Yanga walianza kwa kasi na kufanikiwa kupata magoli kupitia kwa Nahonda wao Bakari Nondo Mwamnyeto dakika 61, huku goli la tatu na la mwisho likifungwa na Mudathiri Yahaya dakika ya 66.

Kwa matokeo haya Yanga wamepanda mpaka nafasi ya pili kwenye kundi lao wakiwa na alama 5 sambamba na Al Ahly , huku mechi yao ijayo wakija kucheza mwezi wa wa pili mwakani dhidi ya CR Belouzidad.

SOMA NA HII  KWA MWENDENDO WA SIMBA ..CHAMA ASHINDWA KUJIZUIA..'ATEMA NYONGO'..ATAKA KURUDI KUOKOA JAHAZI...