Home Habari za Simba Leo SIMBA YAHUSISHWA NA MSHAMBULIAJI HUYU.

SIMBA YAHUSISHWA NA MSHAMBULIAJI HUYU.

Habari za Simba leo

INAELEZWA kuwa Simba ipo kwenye mazungumzo ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Ihefu FC ambayo kwa sasa inaitwa Singida Black Stars, Ismail Mgunda.

 

Nyota huyo Mgunda anayewaniwa vikali na Red Devils ya nchini Ghana ambayo inahitaji saini yake akapate changamoto mpya.

 

Mgunda ndiye alikuwa anaunda safu nzuri ya ushambuliaji pamoja na Elvis Rupia katika kikosi cha Singida Black Stars katika msimu wa 2023/24 uliogota mwisho huku Yanga wakiwa ni mabingwa.

 

Simba imepanga kukiboresha kikosi chao, ili kifanye vema katika msimu mpya wa 2024/25 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote.

 

Miongoni mwa sehemu ambazo zitafanyiwa maboresho ni ile safu ya ushambuliaji ambayo haijawa kwenye uimara ndani ya 2023/24 huku kinara akiwa ni Saido Ntibanzokiza ambaye alifunga mabao 11.

 

Taarifa zimeeleza kuwa Simba ipo katika mazungumzo ya mwisho na mshambuliaji huyo, ambaye yupo katika rada za kusajiliwa na Red Devils inayoshiriki Ligi Kuu ya Ghana.

 

Simba imekuwa ikifanya mambo yake   kimya kimya huku, watu wengine wakijua klabu hiyo ina migogoro, kumbe ni mchezo ambao wameamua kuucheza ili kuwapoteza maboya maadui zao.

 

Mpaka sasa Simba imekamilisha sajili kadhaa za wachezaji muhimu, kuna  Elie Mpanzu, Serge Pokou, Lameck Lawi na Yusuph Kagoma, huku baadhi  ya majina yakiwa yamefika mezani kwaajili ya kusajiliwa kama Steve Mukwala na mengine.

SOMA NA HII  KAMA UTANI VILEE...AZAM FC WAHAMIA SIMBA SC...KAKOLANYA 'AUNDIWA KAMATI'....