Home Uncategorized ISHU YA AJIBU KUSEPA SIMBA IMEFIKIA HAPA

ISHU YA AJIBU KUSEPA SIMBA IMEFIKIA HAPA


BAADA ya hivi karibuni kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu kudaiwa kupata dili la kuwaniwa na moja ya timu kutoka nje ya Tanzania, uongozi wa klabu yake unadaiwa kuwa upo tayari kumruhusu kuendelea na maisha yake.
Imeelezwa kuwa Ajibu amepata dili hilo lakini maambukizi ya Virusi vya Corona yamekuwa kikwazo kwake kukamilisha mchakato wa mazungumzo ya usajili, hivyo inasubiriwa janga hilo limalizike ili kila kitu kiendelee.
  
Mmoja wa viongozi wa Klabu ya Simba alisema:-“Kama amepata timu ya kucheza nje ya nchini sisi hatuna kizuizi, hatuwezi kumzuia.

“Tangu atue katika kikosi chetu amekuwa akipata wakati mgumu katika kikosi cha kwanza, kama kuna timu amepata ije tutazungumza vizuri tu,” alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe kuwa kuwa siyo msemaji wa klabu.
Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa ili azungumzie hilo hakupatikana.Upande wa Meneja wa Ajibu, Rahim Abbas alisisitiza kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo na lingine lolote kwa kuwa afya yake haiko vizuri.

Chanzo: Championi
SOMA NA HII  KUMBE! SIMBA ILIKUWA IMEPANGA KUCHEZA NA WAARABU