Home Uncategorized KUMBE! SIMBA ILIKUWA IMEPANGA KUCHEZA NA WAARABU

KUMBE! SIMBA ILIKUWA IMEPANGA KUCHEZA NA WAARABU

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa mpango mkubwa kwenye mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki kilele cha Simba day ilikuwa kucheza na waarabu wa Misri, timu ya Al Ahly ila imeshindikana kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Agosti 19, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mipango yao ilikwama kutokana na uwepo wa janga la Corona ambalo limevuruga ratiba nyingi duniani.

“Tulipanga kucheza na Al Ahly lakini changamoto ya janga la Virusi vya Corona imefanya jambo hilo kuwa gumu. Tulijitahidi kwenda mpaka Zambia huko ila nako hali ilikuwa namna hivyohivyo ndio maana tukaenda Burundi.


“Tunaamini Vital’O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo maana hata nao pia ilikuwa ngumu kuwapata lakini kutokana na ukubwa wa timu ya Simba basi wamekubali ombi letu na tutacheza nao Uwanja wa Mkapa,” amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 jioni na milango Uwanja wa Mkapa kutakakochezwa mchezo huo na ule Uwanja wa Uhuru ambapo kutakuwa na ‘Big Screen’ itafunguliwa majira ya saa mbili asubuhi.
SOMA NA HII  KOCHA MKUU WA BARCELONA AKALIA KUTI KAVU