Home Uncategorized NYOTA HUYU KIPENZI CHA MASHABIKI ATAJWA KUREJEA JANGWANI

NYOTA HUYU KIPENZI CHA MASHABIKI ATAJWA KUREJEA JANGWANI

INAELEZWA kuwa miongoni mwa washambuliaji ambao wanahitajika kurudi ndani ya Klabu ya Yanga ni pamoja na staa wao wa zamani, Heritier Makambo anayekipiga Horoya.

Msimu wa 2018/19 Makambo alifanya kazi kubwa ndani ya Yanga akiwa ametupia mabao 17 huku kinara akiwa na Meddie Kagere aliyetupia mabao 23.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kuhusu suala la Makambo muda utazungumza kwani ni mchezaji anayependwa na Yanga.

“Makambo ni mchezaji mzuri na anapendwa hivyo hilo ni suala la kusubiri na kuona mambo yatakuaje, ila kwa sasa tuache bado muda wake haujafika,” amesema.

SOMA NA HII  HAWA HAPA NDIO WAPINZANI WA SIMBA,YANGA KIMATAIFA