Home Habari za Simba Leo BREAKING NEWS: SALIM TRY AGAIN AJIUZULU SIMBA…MO DEWJI KUCHUKUA NAFASI

BREAKING NEWS: SALIM TRY AGAIN AJIUZULU SIMBA…MO DEWJI KUCHUKUA NAFASI

habari za simba leo

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Salim Abdallah Try Again ametangaza kuachia nafasi yake, n kumuomba Muwekezaji wa timu hiyo Mohammed Dewji kuchukua nafasi yake.

Salim Try Again amefikia uamuzi huo baada ya yanayoendelea katika klabu hiyo kwa siku za hivi karibuni, hivyo kutoka na kuiongoza Simba kwa miaka 7 sasa ni wakati wake wa kuachia wengine.

“Nimemuomba Mohammed Dewji aje kuwa Mwenyekiti wa Bodi kama atakubali, nimekubali na kwa maana hiyo sasa natoka kuwa mwenyekiti wa Bodi, nitabaki kuwa kama mwanachama wa kawaida wa Simba na Mpenzi, na nitaitumikia Simba kwa namna yeyote”

“Mimi ni mdogo kuliko klabu, nimekaa miaka 7 lakini sasa nimeona niachie ngazi hii, niwashukuru viongozi wengine na bodi, hawa waliobaki tuwape sapoti, tuondoe migogoro tuwe nguvu moja, tumpe sapoti Mohammed Dewji” Amesema Salim Abdallah.

Pia aligusia suala la wachezaji wa timu hiyo kuihujumu Simba kwenye mechi zake, na kama Uongozi wameligundua hilo na umeanza kulifanyia kazi jambo hilo, ikiwemo kuwaacha baadhi ya wachezaji.

“Simba akicheza na kimataifa anacheza mpira mzuri, lakini akicheza na Ihefu hawachezi, ni usaliti tumegundua, viongozi tunalifanyia kazi mchezo huu mchafu na hukubaliki kwa klabu yatu”

“Hakuna kiongozi asiyeumia timu yake inapo poteza matokeo, mashabiki wanaumia ila Kiongozi anaumia zaidi, tumepitia kipindi kigumu haswa kwenye vyanzo havikuwa vinatosha, ila niseme Simba itakuwa imara na tutakuwa na wachezaji watakaoukuwa na moyo unafanya vizuri na wengine tutawaacha”

Akizungumzia usajili mbovu kwa miaka 3 nyuma alisema usajili ni gambling/kamari lakini mashabiki wa Simba wamekuwa wanatabia wa kushinikiza.

“Usajili ni kamari, unaweza kusajili wasifanikiwe, msimu tumesajili wachezaji wengi, Aubin Kramo ana matatizo lakini wengine wanacheza, tumemsajili Jobe na Fredy wanahitaji kuzoea mazingira”

“Hata hao wenzetu wanasajili wachezaji wengi lakini sio kwamba hawakosei, utaratibu wao na wetu ni tofauti, sisi kwakuwa hatuna mafanikio tunasemana sana, ila wao mafanikio yanawabeba”

“Nimeitumikia Simba kwa muda mrefu takribani miaka 7 ndani ya klabu ya Simba SC tangu mwaka 2017”

“Wakati nnachukua nafasi ya kuwa kiongozi Simba,niliichukua ikiwa kwenye hali ngumu, haikuwa na ofisi, ilikuwa na mabasi mawili tu, watumishi walikuwa 5 tu sasa hivi wapo zaidi ya 60, na nafasi kimataifa ilikuwa chini sana, wakati ule mazoezi tulikuwa unafanya uwanja wa kinesi”- Salim Abdallah

“Nimeingia Simba tulikuwa tunachangishana, Mo Dewji alikuwa anatoa Milioni 10, na Mimi nilikuwa nachangia Milioni 10 kwa miaka hiyo, kwa sasa tumepiga hatua kubwa chini ya MO, Simba ni mfano wa vilabu vingine, tumefanya jitihada kubwa kuifanya Simba kuwa bora”

SOMA NA HII  MAYELE NA MUSONDA WAMPA JEURI RAISI...YANGA ITAWEKA REKODI MSIMU HUU...TIMU IPO VIZURI