Home Habari za Simba Leo MANGUNGU NA TRY AGAIN WAGOMA KUJIUZULU…SIMBA MOTO UNAWAKA

MANGUNGU NA TRY AGAIN WAGOMA KUJIUZULU…SIMBA MOTO UNAWAKA

HABARI ZA SIMBA LEO

HABARI ZA SIMBA LEO; Iko wazi sasa Mwenyekiti wa klabu hiyo Murtaza Mangungu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ wamesema hawana mpango wa kujiuzulu nafasi zao sambamba na Wajumbe wa Bodi upande wa Wanachama.

Hayo yamekuja siku chache baada ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba upande wa Mwekezaji, kuridhia uamuzi wa Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji aliowataka kuachia ngazi.

Wajumbe wanne upande wa mwekezaji walioachia ngazi ni Dk Raphael Chegeni, Hamza Johari, Zulfikar Chandoo na Rashid Shangazi.

Akizungumzia hilo, Seleman Haroub ambaye ni Mjumbe wa Bodi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Simba, amesema wajumbe wote wa Bodi hiyo upande wa wanachama wakiongozwa na Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu hawajajiuzulu nafasi zao na hawafikirii kufanya uamuzi huo.

Hayo aliyasema katika kikao cha viongozi wa matawi wa wilaya kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani ya Pwani na Morogoro kilichofanyika Juni 8, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Tulikuwa na kikao na viongozi wa matawi wa wilaya Mkoa wa Dar es Salaam lakini pia walikuwepo wengine kutoka mikoa ya jirani kama Pwani na Morogoro.

“Kubwa zaidi ni kwamba tulipenda kuzungumzia mambo yanayoendelea ndani ya klabu ambapo kuna watu wamejiuzulu na wengine wakisema kwamba viongozi wote wa Bodi wamejiuzulu.

“Wanachama wanapaswa kuelewa kwamba sisi viongozi wa Bodi hususani upande wa wanachama hatujajiuzulu na hatuoni sababu ya kujiuzulu. Sisi tupo na tunaendelea na majukumu yetu kama kawaida kwa mujibu wa katiba yetu na taratibu nyingine za Bodi ya Simba.

“Lakini pia hata wenyeviti wetu ambao sasa wamesafiri nje ya nchi, Mwenyekiti wa Bodi, Salim Abdallah ‘Try Again’ na Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu tunawasiliana nao kwa simu na wametoa matamko kwamba hawajajiuzulu na hawatajiuzulu.”

SOMA NA HII  ANTHONY TRA BI TRA AWINDWA NA SIMBA...NI BEKI WA KATI