Home Uncategorized HIKI NDICHO KINACHOIMALIZA KMC KUSHINDWA KUPATA MATOKEO CHANYA, DAWA YAKE YAPATIKANA

HIKI NDICHO KINACHOIMALIZA KMC KUSHINDWA KUPATA MATOKEO CHANYA, DAWA YAKE YAPATIKANA


 HARUNA Harerimana, Kocha Mkuu wa KMC amesema kuwa kazi kubwa aliyonayo kwa sasa ni kusuka upya kikosi kitakachowavuruga Mtibwa Sugarambao ni mabingwa wa kombe la Mapinduzi.
Hererimana amechuka mikoba ya Jackson Mayanja ambaye alitimuliwa ndani ya kikosi hicho kutokna ana timu hiyo kutokuwa na matokeo bora alijiunga na KMC akitokea timu ya Lipuli ya Irnga.
Harerimana amesema kuwa alitumia muda mwingi kutazama CD za KMC kabla ya kuanza kuifundisha na tatizo kubwa alilogundua ni uvivu wa wachezaji kushindwa kukaba na kutumia nafasi wanazozipata.
 “Baada ya kufuatilia vizuri katika michezo yao iliyopita niligundua kuwa timu imekuwa haichezi vizuri pale inapotokea imepoteza mpira hivyo kuwapa nafasi wapinzani kuleta madhara langoni nimekuja na program maalumu ambayo itawafanya vijana wawe imara na kupata matokeo kwenye mechi zetu zote,”  amesema Harerimana.
KMC ipo katika nafasi ya 17 kwenye  msimamo wa Ligi kuu Bara ikijikusanyia alama 14, imeshinda michezo mitatu, imefungwa mechi nane na kutoa sare katika mechi tano.

SOMA NA HII  YAI LAIPONZA DODOMA FC YAKAMULIWA MKWANJA WA KUTOSHA, ALIYEMTEMEA MATE MWAMUZI APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU