Home Habari za michezo BENCHIKHA AREJESHA MATUMAINI MAPYA SIMBA

BENCHIKHA AREJESHA MATUMAINI MAPYA SIMBA

Habari za Simba leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchikha amerejesha matuamini kwa mashabiki wa timu hiyo na amekabidhiwa faili la Jwaneng Galaxy ya Botswana ambao watakutana nao Jumamosi hii katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka leo nchini kuelekea Botswana kwa ndege ya kukodi na tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao hawataki kurudia makosa ya mwaka 2021 kwa kushinda ugenini kwa mabao 2-0 na kuja kupoteza nyumbani uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mabao 1-3.

Kocha huyo amesema kazi kubwa ni kufanyia kazi mechi iliyopo mbele yao kwa kusahihisha makosa yao lakini pia kufanyia kazi ubora wa wapinzani wao ambao wamewaona katika michezo yao.

Ameelema amekutana na walimu walikuwa na jukumu la kuongoza timu hiyo kipindi bado hajapewa jukumu la kukinoa kikosi hicho kwa kuwaeleza walipoanzia na walipofikia na kukabidhiwa masuala yote na kuendelea alipoishia ili kwenda kusaka matokeo chanya ugenini.

“Nimewakumbusha wachezaji majukumu yao na kuhakikisha wanajituma ili kuwapa furaha mashabiki, ninawaamini kwa pamoja tunaweza kubadili hali ya hewa iliyopo sasa na kurudisha furaha na kuanza kupata ushindi.

Ni kweli kuna mechi mbele yetu kazi tumeanza kuifanya, wachezaji wanaelewa nini wafanye tunahitaji kushinda hiyo mechi, kila mmoja anatakiwa kujituma kwa ajili ya timu na kutumikia nembo ya klabu,” amesema kocha huyo.

Amesisitiza kuwa kuhitaji mchezaji ambaye anajituma na kufanya majukumu yake na hatakuwa tayari kumvumilia mchezaji youote ambaye atakwamisha majukumu yake.

Benchikha ameanza anatambua ugumu michuano ya ligi ya mabingwa lakini anaimani wachezaji wakiamua kujitoa na kupambania klabu watafanikiwa katika malengo yao ua kutwaa mataji na kuvuka robo na kwenda kucheza nusu fainali ya ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA KUWAVAA WAARABU LEO....JEURI YA YANGA LEO IKO HAPA ....