Home Habari za Simba Leo MAPYA YAIBUKA SIMBA…CHAMA ATIBUA DILI LAKE…INSHU IKO HIVI

MAPYA YAIBUKA SIMBA…CHAMA ATIBUA DILI LAKE…INSHU IKO HIVI

Habari za Simba SC

KIUNGO Mzambia Clatous Chama ameendelea kuweka ngumu kwenye kuongeza mkataba mpya na klabu yake ya sasa Simba SC.

Inaelezwa kwamba Uongozi wa Simba SC unapambana sana kumshawishi Chama asaini mkataba hata wa mwaka mmoja tu, kuendeleea kukipiga kwenye klabu ya Simba.

Sababu ya Chama zinazomfanya aweke ngumu kusaini mkataba mpya, Soka la Bongo linafahamu kwamba mchezaji huyo anataka kuboreshewa maslahi yake.

Chama ameuambia Uongozi wa Simba anataka aongezwe dau lake la usajili, na alipwe mshahara wa dola 200,000/= sawa na zaidi ya Tsh Milioni 50 zaidi ya hapo hawezi kusaini mkataba mpya.

Awali mshahara kama huo alikuwa analipwa Luis Miquissone ambaye Simba wameachana nae, na kwa upande wa Chama anataka mshahara mkubwa kuliko mchezaji yeyote Simba.

Hata hivyo inasemekana mcheezaji huyo kuna timu moja kutoka Kariakoo imemuwekea ofa nzuri zaidi kuliko ya Simba, na huenda akasainiwa huko.

Habari za Simba leo zinaeendelea kushika kasi, kuanzia kwenye sakata lao na beki wa kati Lameck Lawi aliyewekewa ngumu na Uongozi wake wa Coastal Union, pia inshu ya Chama nayo imeibuka.

Mashabiki wa Simba wameonekana kuchoka mizengwe za mchezaji huyo kwa kila msimu, ukizingatia amekuwa akihusishwa na utovu wa nidhamu kambini na kujiona yeye ni mkubwa kuliko Simba, sasa wengi wao wanasema bora Simba waachane na mchezaji huyo, ila watengeneze timu itakayocheza bila kumtegemea Chama na itakayodumu kwa muda mrefu.

Je nini kitatokea zaidi, endelea kusalia nasi kwa taarifa za uhakika na kina.

SOMA NA HII  KIBOKO YA SIMBA NA YANGA AVUTIWA WAYA AZAM FC