Home Uncategorized YANGA YAMPA MKATABA KIPA AKIWA MISRI

YANGA YAMPA MKATABA KIPA AKIWA MISRI


MABOSI wa Yanga baada ya kusikia kwamba Azam FC wanamnyemelea kipa Metacha Mnata, wameamua kumpa mkataba kipa huyo fasta akiwa Misri.

Yanga wanapambana vya kutosha kuhakikisha wanampata Metacha baada ya kushindwa kukamilisha kwa wakati dili lake akiwa kwenye kambi ya Taifa Stars jijini Dar es Salaam. Wakati Yanga wakiwa kwenye harakati hizo za kumchukua Metacha, Azam FC nao wamefuata kipa huyo ambaye yupo na Taifa Stars nchini Misri.

Azam wanataka kumrudisha nyumbani Metacha ambaye walimtoa kwa mkopo
kwenda Mbao FC baada ya kupata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika pia wapo njiani kumuondoa kipa Mghana Razack Abalora.

Taarifa zinasema kwamba Yanga wameamua kwenda kukamilisha dili hilo nchini Misri baada ya kuona Azam wameanza harakati za kumsajili.

“Kila kitu kilikuwatayari hapa nchini juu ya kumsajili lakini baada ya hizi taarifa za Azam kumtaka, basi Yanga wameona waende kumaliza kila kitu huko Misri. “Kinachofanywa ni kwamba akirudi hapa Dar ajiunge tu na timu moja kwa moja,” kilisema chanzo chetu ndani ya Yanga.

“Mpaka sasa nimezungumza na Yanga ambao ndiyo tulikuwa vizuri na mazungumzo ila sikusaini mkataba. “Tulikuwa na vitu kadhaa havijakamilika ila nadhani vinaweza kuisha wakati nikirudi baada ya kutoka Misri.” Dili hilo la Metacha na Yanga linashindwa kukamilika hadi sasa kutokana na kipa huyo kubakiwa na miezi miwili katika mkataba wake na Azam FC.

SOMA NA HII  AHMED ALLY ANAJUA KUWA YANGA IMEBADILIKA ILA MSIMAMO WA SIMBA NI HUU