Home Uncategorized USAJILI WA WACHEZAJI WA NJE NI LAZIMA, LAKINI LAZIMA MUWE NA MIPANGO...

USAJILI WA WACHEZAJI WA NJE NI LAZIMA, LAKINI LAZIMA MUWE NA MIPANGO BORA KWA TIMU ZA VIJANA





NA SALEH ALLY
WAKATI huu ndio ule ambao gumzo zaidi ni kuhusiana na usajili wa wachezaji wapya ambao msimu ujao watakuwa na klabu zao kwa ajili ya mismo mpya.


Wako watakuwa ni wageni kabisa wa Ligi Kuu Bara lakini wako ambao watakuwa wenyeji wa ligi hiyo lakini wako katika timu nyingine mfano wa Salim Aiyee ambaye amekwenda kujiunga na KMC akitokea Mwadui FC.


Simba na Yanga, ndio zimekuwa gumzo zaidi ya timu nyingine katika hilo la usajili, hii inachangiwa na ukubwa walionao katika mpira wa Tanzania. Ni klabu zenye watu wengi zaidi wanaoziunga mkono.


Ukiachana na watu wengi, ukongwe wake katika mchezo wa soka nchini, lazima zitakuwa gumzo ukilinganisha na klabu nyingine kama litafikia suala la usajili.


Ukiangalia suala la wachezaji wanaosajiliwa kutokea nje ya Tanzania, Simba na Yanga wamekuwa wakisajili kwa wingi zaidi wachezaji kutoka nje na hili hata kama ni marengo ya timu lakini imekuwa ni burudani ya kukonga nyoyo kutoka kwa mashabiki.


Wakati mashabiki wakiwa wanafurahia, Simba na Yanga lakini pia klabu nyingine kama Azam FC, sasa KMC na nyingine baadhi zimekuwa zikimwaga mamilioni ya fedha nje ya Tanzania kwa ajili ya kusajili wachezaji wapya kutoka nchi mbalimbali duniani.


Suala la kusajili wachezaji kutoka nje ya Tanzania halikwepeki, ni suala la limpiar na linafanyika kila sehemu, hivyo si dhambi lakini lazima kuwe na hesabu ya kupambana na suala hili ili siku moja lisie kutengeneza udhoofu utakaifanya Tanzania ishiriki biashara ya kununua tu bila ya kuuza.


Tanzania ina uwezo wa kununua wachezaji 30 wa kigeni kupitia timu tatu tu ambazo ni Simba, Yanga na Azam. Lakini ziko zinazoweza kujitutumua na mwisho wachezaji wa kigeni wakafikia hadi 50. Wakati huohuo kunakuwa hakuna uwezo kwa timu za Tazania kwa ujumla kuuza hata wachezaji 15 kwa msimu mmoja kwenda nje ya Tanzania.


Hivyo ukubwa wa manunuzi kutoka nje kuingia ndani unaweza kuwa mkubwa sana huku uuzaji kutoka ndani kwenda nje ukawa wa kiwango duni kabisa ambao unaifanya Tanzania kuwa bora katika ununuaji tu, hili ni tatizo.


Tunaonunua kwao wana mambo kadhaa walifanya tukaona. Kwa wachezaji kutokea nchi kubwa kama Brazil tunajua, ni nchi imejijenga na kujitangaza kupitia soka na hata wachezaji wao, iwe kiwango kikubwa au kawaida tu, thamani yao itakuwa juu.


Ukiachana na hao, nyota wa Kenya, Uganda, Rwanda na kadhalika leo wanaona Tanzania ndio sehemu sahihi ya kuchuna. Wachezaji hadi kutoka nchini Sudan wameanza kuja nchini kwa kuwa kunalipa.


Hili la wao kuja hasa kama wakiwa na viwango sahihi vya ushindani, itakuwa na faida kubwa. Wataongeza changamoto ya ushindani lakini changamoto ya kuamsha vichwa vyetu kuanza kufikiria upya kuhusiana na suala la nini tunanye kwa ajili ya badayee.


Kazi ya kukuza vipaji na kuviendeleza ni muhimu sana. Ndio maana nikaona suala la usajili kwa mamilioni ya fedha ni vizuri sana lakini suala la kuanza kuwajenga watoto na vijana litakuwa bora zaidi.


Ubora wake utatokana na faida mbili. Kwanza ni kuwauza watoto wanaochipukia wakiwa katika viwango bora. Wanaweza kuuzwa hapa nchini au ikiwezekana nje ya Tanzania halafu klabu ikaanza kufaidika watakapoendelea kuuzwa katika klabu nyingine zikiwemo zile zenye fedha nyingi zaidi.


Pili ni faida kwa timu zenyewe, wakati mwingine badala ya kumwaga mamilioni ya fedha kununua mchezaji Kenya au Uganda, zinaweza kuwapandisha wachezaji wakafanya vizuri na baadaye kuitangaza klabu na nchi na biashara ikafanyika.


Hili suala la kukuza na kuendeleza vipaji zaidi lile la Klau. Tuachane na kuilalamikia TFF kwamba haikuzi na kuendeleza. Yenyewe isimamie mchakato huo na taratibu zake lakini inaweza kusaidia pia kwa kusimamia mashindano kadhaa yatakayoonyesha vipaji vya vijana kama yale ya U15 Youth League, Copa 17 na U20 Premier League ambayo wamekuwa wakiyasimamia.

Kusajili kwa wingi kutoka nje kama nilivyosema ni suala zuri lakini lazima tuone linaweza lisiwe na suluhisho la muda mrefu. Klabu zisajili lakini zilishikilie kwa nguvu kubwa suala la watoto na vijana ambao baadaye watakuwa msaada mkubwa.

Kuna uwezekano Kama litashikiliwa na kupewa kipaumbele, siku moja Simba au Yanga au Azam FC zinaweza kufika mbali zaidi katika michuano iliyo chini ya Caf huku zikiwa na mgeni mmoja au wawili pekee.

Tumeona nchi nyingi za Afrika Kaskazini kutoka katika nchi kama Tunisia, Algeria, Morocco na Misri zimekuwa zikifanya vizuri huku zikiwa na mchezaji mmoja au wawili tu tokea nje ya nchi zao na hili linatokana na program bora na uwekezaji sahihi kwa watoto na vijana.



SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO AZAM FC MAMBO SAFI

1 COMMENT

  1. You could certainly see your expertise in the article you write.
    The sector hopes for more passionate writers like you who aren’t afraid to say how they believe.
    Always go after your heart.

    Here is my page :: exterior front doors