Home Uncategorized LIVERPOOL YATHIBIITISHA SADIO MANE KUIKOSA MANCHESTER CITY

LIVERPOOL YATHIBIITISHA SADIO MANE KUIKOSA MANCHESTER CITY

 JURGEN Kloop, Meneja wa Liverpool amesema Sadio Mane ataukosa mchezo wa Ngao Jamii (Community Shield) dhidi ya Manchester City uwanja wa Wembley Agosti 4.

Mane ataukosa mchezo huo baada ya kupewa likizo ya wiki mbili kutokana na kushiriki michuano AFCON nchini Misri, timu yake ya Senegal ilifika fainali na kufungwa bao 1-0 na Algeria.


Mane ataiunga na klabu hiyo Agosti 5 siku moja baada ya mchezo huo. “Kwa sasa yupo mapumziko, tumempa likizo ya wiki mbili. Na anatarajia kurudi hapa Agosti 5 siku moja baada ya mchezo wetu na Manchester City. 


“Atakuwa na siku nne au tano za kujiandaa na mchezo dhidi ya Norwich na siku 10 mchezo dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa UEFA SUPER CUP”amesema.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KIWANGO KIKUBWA..STARS YABAKI PALEPALE FIFA