Home Uncategorized RUVU SHOOTING:TUTAWASHANGAZA WENGI KESHO

RUVU SHOOTING:TUTAWASHANGAZA WENGI KESHO

OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa kesho watawashangaza wengi ndani ya uwanja kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.

Ruvu Shooting itamenyana na Simba Uwanja wa Taifa ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema: “Tutawashangaza wengi kesho kwa kuonyesha soka makini kwani maandalizi yapo sawa naona wengi wametusahau ila tupo tayari,” amesema.

Ruvu Shooting ilifungwa mabao 3-0 mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

SOMA NA HII  NAFASI YA HAJI MANARA SIMBA YAGOMBEWA KWA KASI YA KUTISHA