Home Azam FC KIROHO SAFI TU…..AZAM FC WAKUBALI KUACHANA NA DUBE….MASHARTI YAO KWA YANGA NI...

KIROHO SAFI TU…..AZAM FC WAKUBALI KUACHANA NA DUBE….MASHARTI YAO KWA YANGA NI HAYA TU…

Habari za Michezo

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa hauna taizo na mchezaji wao Prince Dube ambaye anahitaji kuondoka ni machaguo mawili anayo kuyafanya kwa sasa kuendelea na maisha yake ya soka bila tabu.

Ipo wazi kwamba Dube ndani ya ligi kwa msimu wa 2023/24 kafunga jumla ya mabao saba anatajwa kuwa kwenye hesabu za kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Machi 4 2024 uongozi wa Azam FC kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,Zakaria Thabit, Zakazakazi alibainisha kuwa wamepokea barua ya mchezaji Dube kuomba kuvunja mkataba wake.

Kiongozi huyo amesema: “Tumepokea barua ya mchezaji wetu Prince Dube kuomba kuvunja mkataba wake hilo tunalijadili na tunalifanyia kazi lakini hakuna tatizo yupo huru kwenda anapotaka yeye.

“Mkataba wake aliongeza kabla ya msimu kuanza ambapo unatarajiwa kuisha 2026 hivyo anachopaswa kufanya ni kutimiza masharti ambayo yapo kwenye mkataba kwa kulipa dola za kimarekani laki tatu ama timu inayomtaka kuja kuzungumza na uongozi.

“Lakini timu ikija bado itapaswa kulipa dola za kimarekani lakini tatu ama chaguo la pili kwa mchezaji ni kubaki ndani ya Azam mpaka mkataba wake utakapoisha atakuwa huru kuondoka,”.

SOMA NA HII  RAISI WA HESHIMA SIMBA...MO DEWJI AMSAMEHE HAJI MANARA..."NIMEMSAMEHE