Home Uncategorized HII HAPA SABABU YA YANGA KUMSAJILI KOTEI MSIMU UJAO

HII HAPA SABABU YA YANGA KUMSAJILI KOTEI MSIMU UJAO

YANGA imerahisishiwa kazi ya kumnasa kiungo wa zamani wa Simba, James Kotei baada ya mchezaji huyo kuvunja mkataba wake na timu yake ya  FC Slavia Mozyr inayoshiriki Ligi Kuu ya Belarus.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.ghanasoccernet.com, mkataba huo wa Kotei (26) na FC Slavia Mozyr umevunjwa kwa makubaliano binafsi baina ya pande hizo mbili.

Sababu kubwa inayoonekana kuchangia kuvunjwa kwa mkataba huo ni kitendo cha Kotei kusgua benchi tangu alivyojiunga na timu hiyo mwezi Januari akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

Katika kipindi cha miezi mitano aliyoichezea Mozyr, Kotei hakuwahi kuanza katika kikosi cha kwanza hata mara moja huku akikaa benchi mara tatu katika mechi 13 ambazo timu hiyo imecheza.

Kitendo cha Kotei kuvunja mkataba huo, ni wazi kinaiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kumnyakua baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu.

Tetesi zinadai kuwa Yanga imefanya mazungumzo mara kadhaa na Kotei na kufikia pazuri ingawa changamoto kubwa ilikuwa ni mkataba wake na Mozyr.

Kotei alitamba vilivyo pindi alipoitumikia Simba kuanzia mwaka 2016 akiiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara mbili, ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam mara moja lakini pia kuisaidia kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/2019.

SOMA NA HII  NDOTO ZA KAHEZA NI KUKIPIGA NJE YA BONGO