Home Uncategorized KAGERE – WATU WANACHONGA SANA JUU YANGU

KAGERE – WATU WANACHONGA SANA JUU YANGU

KINARA wa mabao wa Ligi Kuu Bara, Meddie Kagere amesema kuwa inaweza kutokea kwa straika yeyote kucheza mechi hata tano bila kufunga bao ila anachoangaliwa yeye ni kipi ambacho anakifanya uwanjani.

Kagere anasema ameshangazwa na maneno ya mashabiki baada ya sare dhidi ya Ruvu Shooting. Alisema baadhi ya mashabiki kwenye mitandao ya kijamii walikuwa wakimueleza maneno makali kwa maana ya kucheza dakika 90, bila kufunga bao katika mchezo huo.

“Huwa nashangaswa sana na mashabiki wetu, kwanza ambalo hawafahamu mpira ndio kazi yangu kwa maana hiyo kushindwa kufanya vizuri kuna vitu vya msingi kama posho huwa nakosa, kwa maana hiyo sitamani kuona nashindwa kufanya vizuri uwanjani,” alisema.

“Kwahiyo huwa napambana kuhakikisha nafunga bao au nikishindwa kufanya hivyo huwa najitahidi kuasisti wenzangu kufunga ndio maana tunacheza kwa ushirikiano na jambo kubwa kwangu si mimi kufunga bali matokeo ya timu.

“Tofauti na maneno hayo ya mashabiki ambayo hutokea mara baada ya timu kushindwa kupata ushindi, nimejiwekea malengo ambayo napambana ili kuyafikia.

“Msimu uliopita nilimaliza ligi nikiwa na mabao 23, ambayo kwanza natamani kuyafikia hayo katika mechi zetu tulizobaki nazo na baada ya hapo ndio nitakuwa na malengo mengine kwa maana ya kufunga mabao zaidi,” alisema.

“Changamoto kwangu katika kipindi hiki ni kwamba tunanza ligi kwani tulikuwa nje ya uwanja kwa muda wa zaidi ya miezi miwili,” alisema staa huyo wa Rwanda mwenye asili ya Uganda.

SOMA NA HII  BEKI KISIKI WA YANGA MALI YA POLISI TANZANIA