Home Uncategorized BOB HAISA AREJEA NA PENZI LA KARAHA

BOB HAISA AREJEA NA PENZI LA KARAHA


BOB Haisa, msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye anaimba mtindo wa mduara amesema kuwa amerejea tena kwenye fani hiyo akiwa na kigongo kipya ambacho anaamini kitamrejesha kwenye chati.

Ngoma yake ya ‘Nipe Mgongo’ ilimpa mafanikio makubwa na kumfanya ajulikane nje na ndani ya nchi kwa sasa kigongo chake kipya kinaitwa Penzi la Karaha.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bob Haisa amesema kuwa ni wimbo mzuri ambao una ujumbe kwa kila anayependa muziki mzuri.

“Kazi nzuri kwa watu wazuri na nimerejea kwa mtindo wa kipekee kwani uwezo wa kuimba na kuandika upo hivyo ni kazi kwa mashabiki kupata kile wanachokipenda,” amesema.


SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA ALHAMISI