Home Uncategorized NYOTA WA MTIBWA SUGAR AJICHIMBIA FUKWENI KUPIGA MATIZI

NYOTA WA MTIBWA SUGAR AJICHIMBIA FUKWENI KUPIGA MATIZI

ABDULHAMAN Humud, nyota anayekipiga Mtibwa Sugar amesema kuwa anaendelea kupiga mazoezi kwenye fukwe li kulinda kipaji chake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Humud amesema kuwa kwa wakati huu wa kujikinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona,amekuwa akifanya mazoezi yake binafsi ili kulinda kipaji.

“Mimi nipo vema na ninaendelea na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ila ninaendelea kufanya mazoezi binafsi ili kuwa bora kwa kufuata program ambayo nimepewa na Kocha Mkuu.

“Mazoezi yangu nayafanya ufukweni kwa kuwa ninahitaji kulinda kipaji changu na pia ninapenda kuchukua tahadhari kwani Virusi vipo na ni muhimu kuchukua tahadhari,” amesema.

SOMA NA HII  SINGIDA UNITED YAIPA SOMO LA KUTOSHA DODOMA FC