Home Habari za michezo KUELEKEA SIKU YA WANANCHI….MWANAYANGA SIKIA KAULI HII YA KIBABE KUTOKA KWA MTAALAMU...

KUELEKEA SIKU YA WANANCHI….MWANAYANGA SIKIA KAULI HII YA KIBABE KUTOKA KWA MTAALAMU AUCHO…


Mchezaji wa kimataifa wa Uganda anayecheza kwenye klabu ya Yanga, Khalid Aucho ameahidi kuwa kuelekea msimu ujao wanatarajia kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya kimataifa.

Aucho kwenye msimu uliopita alichezea Yanga michezo 21 na kufanikiwa kufunga bao moja na kutoa asisti tatu kwenye michezo yote aliyoicheze klabu hiyo.

“Msimu uliopita hatukuwa fiti sana ndio maana hata kwenye michuano ya kimataifa tulitolewa katika hatua ya awali.

“Msimu ujao tunawaahidi wana yanga kwamba tutafanya vizuri kutokana na maandalizi ambayo tumefanya hata kama ni kwa kipindi hiki kifupi ambacho tumejiandaa kinatosha sana.

“Wachezaji ambao wameongezwa kwenye kikosi wataongeza kitu na tutafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita.”

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA KUANDIKA REKODI MPYA