Home Uncategorized MCHEZO MZIMA WA SIMBA KUSEPA NA POINTI TATU MBELE YA MWADUI FC...

MCHEZO MZIMA WA SIMBA KUSEPA NA POINTI TATU MBELE YA MWADUI FC ULICHEZWA KWA MTINDO HUU


SIMBA jana imefuta machungu ya sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Juni 14, Uwanja wa Taifa kwa kuifunga mabao 3-0 Mwadui FC.
Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ambapo kasi ya Simba kuliandama lango la Mwadui ilianza kipindi cha kwanza na dakika ya tisa, Hassan Dilunga alifunga bao la kwanza akimalizia pasi ya John Bocco.
Dakika ya 21 Augustino Samson alijifunga wakati akiokoa krosi iliyomwaga na Shomari Kapombe.
Licha ya Mwadui FC kupambana kutafuta nafasi ya kufunga bao wakimtumia mshambuliaji wao Gerald Mdamu jitihada zake zote zilikwama kwenye ukuta wa Simba uliokuwa chini ya Pascal Wawa na Erasto Nyoni.
Bao la tatu kwa Simba lilifungwa na nahodha wa Simba, John Bocco kwa kichwa dakika ya 58 akimalizia shuti lililogonga mwamba baada ya kupigwa na kiungo wa Simba Luis Miqussone.
Kiungo mshambuliaji anayetumia mguu wake wa kulia Said Ndemla alikuwa kwenye ubora wake ambapo alikuwa akiwasumbua wapinzani wa Mwadui kwa kutoa pasi zilizokuwa na uhakika huku akionekana kuichezesha timu kwa umakini mkubwa.
Ushindi huo unaifanya Simba ijikite kileleni ikiwa na pointi 75 na mabao 67. Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kambarage, Mwadui ilishinda bao 1-0 na kusepa na pointi tatu ambazo jana wameziacha Dar.
Kikosi cha Simba kilichoanza
Aishi Manula,Shomari Kapombe,Mohamed Hussein,Kenned Juma,Pascal Wawa,Erasto Nyoni,Gerson Fraga,Said Ndemla,John Bocco, Luis Miqussone na Hassan Dilunga.
Kikosi cha Mwadui FC
Mahamoud Amour,Mfaume Omari,Yahya Mbengu,Joram Mgeveke,Augustino Samson,Frank John, Joseph,Enrick Nkosi,Raphael Aloba,Gerald Mdamu na Herman Masenga.
SOMA NA HII  HAJI MANARA AIBUKA NA JIPYA SIMBA, AMTAJA BALINYA YANGA, UNAWEZA UKACHEKA - VIDEO