Home Uncategorized NAMUNGO KAMILI GADO KUVAA MBEYA CITY LEO SOKOINE

NAMUNGO KAMILI GADO KUVAA MBEYA CITY LEO SOKOINE


KOCHA wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kupambana leo na Mbeya City kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.

Namungo itashuka Uwanja wa Sokoine saa 10:00 jioni kumenyana na Mbeya City iliyo chini ya Amri Said.

“Wachezaji wana morali kubwa na wanatambua kazi yao ni kutafuta ushindi, utakuwa mchezo mgumu kutokana na ushindani uliopo ila hakuna namna tupo tayari kupambana.

“Kikubwa ni kuomba Mungu wachezaji wafuate kile ambacho nimewaelekeza na wacheze kwa juhudi, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa timu sapoti,” amesema.

SOMA NA HII  KOCHA ANAYETAJWA KUIBUKIA SIMBA KUSHUKA NA JEMBE HILI LA KAZI