Home Uncategorized KESHO AZAM FC MIKONONI MWA IHEFU KULITETEA TAJI LAO LA SHIRIKISHO

KESHO AZAM FC MIKONONI MWA IHEFU KULITETEA TAJI LAO LA SHIRIKISHO


MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Azam FC kesho watakuwa na kibarua cha kuendeleza mbio za kutetea taji lao hilo kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.

Azam FC itakaribishwa na Ihefu, Uwanja wa Sokoine majira yaa saa 10:00 kutafuta tiketi ya kusonga mbele hatua ya robo fainali.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na uimara wa kikosi cha Ihefu kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na uimara wa Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba.

Idd Cheche, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa mabingwa wakiwa ni mabingwa watetezi ni lazima wapambane kulitetea taji lao.


SOMA NA HII  MANE, SALAH KUCHEZA NA SAMATTA