Home Habari za michezo SAKATA LA NTIBAZONKIZA NA AMBUNDO KUSIMAMISHWA…MANARA ASHINDWA KUJIZUIA…NAYE KAIBUKA NA HILI…

SAKATA LA NTIBAZONKIZA NA AMBUNDO KUSIMAMISHWA…MANARA ASHINDWA KUJIZUIA…NAYE KAIBUKA NA HILI…


Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara ameeleza kuhusu kusimamishwa kwa wachezaji wa Klabu hiyo Saido Ntibazonkiza na Dickson Ambundo.

“Ni kweli wachezaji hawa kocha Nabi ameamua kuwasimamisha kwa wiki hii na baadae wakija Dar Es Salaam, watazungumza nae pamoja na uongozi kuona nini kitakachoendelea,” amesema Haji Manara.

“Ni kweli Saido na Mwenzake baada ya kumaizika kwa mchezo dhidi ya Biashara waliondoka kambini na wakarejea alfajiri hivyo kitendo hicho kimemfadhaisha kocha na uongozi wa klabu ya Yanga kwa ujumla,” amesema Haji Manara.

Ntibazonkiza na Ambundo walisimamishwa na Nabi, ambapo pia huenda wakaukosa mchezo wa kesho dhidi ya Simba SC.

Aidha taaria za ndani kutoka Yanga ambazo bado hazijathibitishwa , zinasema kuwa Klabu hiyo ioo kwenye mpango wa kuachana na nyota hao wawili kwa tabia hiyo huku muhanga wa mpango huo akiwa ni Saido Ntibazonkiza ambaye anasadikiwa kufanya vitimbi ili atimuliwe na kukamilisha dili lake la kujiunga na Simba.

Kwa upande wa Ambundo, inasemekana klabu hiyo inampango wa kumtoa kwa mkopo ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine wenye uwezo wa kucheza na nidhamu kwa timu na uongozi kwa ujumla.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZA 'KUIKANDA' SIMBA JANA....AL AHLY 'HAOOO CHAP WASEPA ZAO BONGO'...