Home Habari za michezo BAADA YA KUTUPIA JANA….MAYELE AFUNGUKA ALIYOKUWA AKIPITIA YANGA…

BAADA YA KUTUPIA JANA….MAYELE AFUNGUKA ALIYOKUWA AKIPITIA YANGA…

Habari za Yanga

Mshambuliaji hatari wa Klabu ya Yanga raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, Fiston Mayele amesema kuwa alimisi sana kutetema kutokana na kuwa na ukame wa mabao katika michezo mitano mfululizo ya mashindano akiwa ndani ya klabu hiyo.

Mayele alifanikiwa kufunga jumla ya mabao matatu (Hat Trick) katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1 na kurejea katika kilele cha msiamo wa Ligi Kuu ya NBC.

“Goli la kwanza lilikuwa la mtoto wangu kwa sababu nimepata mtoto mpya ndo maana uliona mechi ya Zalan nikafunga nikaweka mpira humu aaah nilimisi sana mechi tano kuna wengine walisema mwezi mzima sitatetema, leo namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufunga Hat Trick ya kwanza kwenye Ligi ya Tanzania,” alisema Mayele.

Hadi sasa Mayele ana jumla ya mabao 6 akiwa sambamba na nyota wa Klabu ya Simba Moses Phiri pamoja na mshambuliaji wa Namungo FC Reliants Lusajo huku mshambuliaji Sixtus Sabilo akiwa kinara wa mabao hadi sasa akiwa na jumla ya mabao 7.

SOMA NA HII  KISA SIMBA NA MASHINDANO YA SUPER LEAGUE...UWANJA WA MKAPA KUPIGWA MSASA UPYAA...