Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA AZAM…..MANARA KAONA ISIWE TABU…LEO KAIBUKA NA HILI JIPYA…

KUELEKEA MECHI NA AZAM…..MANARA KAONA ISIWE TABU…LEO KAIBUKA NA HILI JIPYA…


Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote za kwenye ligi ikiwa ni pamoja na mchezo wao dhidi ya Azam FC .

Akizungumza na waandishi wa habari Manara amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini wanaamini kwamba watapata ushindi kwenye mchezo huo.

“Tunatambua kwamba mchezo wetu utakuwa mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi na tuna amini kwamba nawezekana mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Haji Manara .

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 48 baada ya kucheza mechi 18 inatarajiwa kukutana na Azam FC Aprili 6, Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  BAADA MAWIMBI MEENGI KUIPIGA SIMBA MSIMU HUU...DEWJI ARUDISHA MAJESHI RASMI SIMBA...TRY AGAIN AINJINIA KILA KITU...