Home Uncategorized YANGA YAIPIGIA MATIZI BIASHARA UNITED

YANGA YAIPIGIA MATIZI BIASHARA UNITED


 BAADA ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC leo kimeanza kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Biashara United. 


Yanga ikiwa chini ya Kaze ambaye ameongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 na kushinda zote kitashuka Uwanja wa Karume, Mara, Oktoba 30.


Mchezo wa kwanza, Kaze alishuhudia kikosi chake kikishinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania na mchezo wa pili kikosi chake kilishinda mabao 2-1. Ndani ya dakika hizo 180 Yanga imefunga mabao matatu na kufungwa bao moja.


Ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 19 na imecheza mechi saba ambapo imefungwa jumla mabao mawili na kufunga mabao 10 na katika hayo mabao 10 ni Waziri Junior pekee ambaye ni mzawa amepachika bao moja huku mengine tisa yakifungwa na wageni.


Kaze amesema:”Bado tuna kazi ya kufanya kwa msimu huu na mechi zetu zijazo, mashabiki waendelee kutupa sapoti na nina amini kwamba kila kitu kitakuwa sawa,” .

SOMA NA HII  OLE GUNNER ACHEKELEA KUCHEZA MECHI 9 BILA KUPOTEZA