Home Habari za michezo KAZE – YANGA TUNAINGIA MIEZI MIWILI YA TABU…TUNA MECHI NGUMU…

KAZE – YANGA TUNAINGIA MIEZI MIWILI YA TABU…TUNA MECHI NGUMU…


Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesisitiza kwamba wamewapa wachezaji ratiba ngumu kwavile miezi miwili ijayo ndiyo fainali yao.

Kaze ambaye muda mwingi hushinda mitandaoni akijifunza mbinu mpya, alisema kwamba kazi yote iliyofanyika tangu mwaka jana sasa ndio inakwenda kufikia kilele na ndio sehemu muhimu sana.

“Hatujawapa wachezaji muda mwingi wa kupumzika kwavile ndani ya miezi miwili ijayo ndio kama fainali ya yale yote tuliyoyaanza mwaka jana, ni miezi yenye mechi muhimu sana,” alisema Kaze

“Tunaingia kwenye mwezi ambao tunacheza na Azam halafu mechi ya FA (Geita) kabla ya Simba hizo zote ni mechi za muhimu kwenye vikombe vyote viwili.

“Kiufundi ni mechi chache sana kwahiyo ukisema uwape uhuru wachezaji, tutatoka kwenye malengo yetu kiufundi maana ni michezo michache sana. Ukitoka mwezi ujao unaingia Mei ambao ni mwezi wa kumalizia kila kitu, sasa unaweza kuona jinsi ratiba ilivyo na umuhimu hivyo tunahitaji kufanya mazoezi ya pamoja kwa muda mrefu pamoja na mechi za kirafiki.

“Tutatumia hizi mechi kuwaweka wachezaji kwenye hali nzuri haswa wale ambao walikuwa majeruhi na wengine hawakuwa na muda mwingi wa kucheza kwenye mechi za ligi, tunataka kufanya mambo yote kwa umakini mkubwa na kuwapa furaha mashabiki wetu,”alisema Kaze ambaye ni raia wa Burundi kama ilivyo kwa Saido Ntibazonkiza ambaye alimsajili yeye.

SOMA NA HII  LICHA YA KUWA HAYUPO....BARBARA AFUNGUKA NAMNA WANAVYOTEMBEA NA MIPANGO, MAWAZO YA PABLO...