Home Uncategorized KICHAPO CHA BAO 1-0 MBELE YA MTIBWA SUGAR CHAFUMUA MIPANGO YOTE SIMBA,...

KICHAPO CHA BAO 1-0 MBELE YA MTIBWA SUGAR CHAFUMUA MIPANGO YOTE SIMBA, CHEKI HESABU ZAO KWA SASA

BAADA ya Simba kulipoteza mara ya pili mfululizo Kombe la Mapinduzi kwa kupokea kichapo cha 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar hesabu zao zimebadilika ghafla na kuhamia kwenye ligi.

2019 Simba ilicheza fainali na Azam FC kwenye Kombe la Mapinduzi na ilichapwa mabao 2-1 na 2020 imeanza kwa kuchapwa bao 1-0 lililofungwa na Awadh Salum dakika ya 39 na kuwafanya wapoteze kwa mara nyingine tena.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa sasa mpango mkubwa ni kufanya vema kwenye mechi za ligi pamoja na mashindano mengine.

“Tumeumia kukosa kombe la Mapinduzi, ni matokeo mabaya kwetu ila hakuna namna maisha lazima yaendelee.

“Kwa sasa nguvu kubwa ni kwenye ligi pamoja na mashindano mengine lazima tupambane kufanya vema,” amesema.

Simba kesho Januari, 16 itashuka uwanjani kumenyana na Mbao FC ya Mwanza, CCM Kirumba.

SOMA NA HII  BREAKING: UCHEBE KURUDI BONGO TENA, AZUNGUMZA KUHUSU SIMBA