Home Uncategorized KMC KUIKAZIA TP MAZEMBE

KMC KUIKAZIA TP MAZEMBE


UONGOZI wa KMC umesema kuwa leo utapambana kupata matokeo chanya mbele ya TP Mazembe kwenye mchezo wa pili wa michuano ya Kagame.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya mchezo wa kupata matokeo.

“Mchezo wetu wa kwanza tulikubali sare haikuwa mpango wetu ila ni matokeo, leo tutapambana kufanya vema hivyo mashabiki wetu wazidi kutupa sapoti,” amesema.

TP Mazembe mchezo wa kwanza alipoteza mbele ya Rayon Sports kwa kufungwa bao 1-0 na KMC ililazimasha sare ya kufungana bao 1-1 na Atlabara FC bao pekee la KMC lilifungwa na Salim Aiyee.

SOMA NA HII  VPL: COASTAL UNION 0-5 SIMBA