Home Uncategorized KUMBE! ROLLERS YAIPELEKA YANGA KILIMANJARO

KUMBE! ROLLERS YAIPELEKA YANGA KILIMANJARO


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa sababu kubwa ya kukimbilia Kilimanjaro kuweka kambi ni mazingira ya mkoa huo kuendana na yale ya nchini Botswana wanakotokea wabaya wao kimataifa Township Rollers.

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa kikosi kimeamua kuweka kambi maalumu Kilimanjaro ili kuendana na hali halisi ya hewa ya wapinzani wao.

“Kikosi kipo vizuri na kambi ya muda itakuwa mkoani Kilimanjaro ambapo huko tutacheza michezo kadhaa ya kirafiki kujiweka sawa.

“Sababu kubwa ya kwenda Kilimanjaro ni mazingira na hali ya hewa ya huko kulingana na ile ya Botswana tunajiaandaa kwa ushindani,” amesema.

SOMA NA HII  VITA YAZIDI KUNOGA KUWANIA SAINI YA MGHANA KATI YA SIMBA NA YANGA