Home Habari za michezo FIFA WAIBUKA NA HILI JIPYA SAKATA LA MABILIONI YA MSUVA KUTOKA KWA...

FIFA WAIBUKA NA HILI JIPYA SAKATA LA MABILIONI YA MSUVA KUTOKA KWA WAARABU….

Habari za Michezo leo

Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiagiza klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kumlipa mchezaji Simon Msuva zaidi ya dola za kimarekani 700,000 (zaidi ya bilioni 1.6 za Kitanzania) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya Wydad.

Wydad, aliagizwa kumlipa pesa hizo Msuva, kabla ya 2022 kumalizika ila Msuva amethibitisha kutolipwa pesa hizo mpaka sasa akiwa yuko huko Saudi Arabia,

Ikiwa CAF watafuata kanuni klabu ya Wydad, itafungiwa kucheza michuano ya CAF kulipa faini pamoja na kupokonywa point au kushushwa katika ligi kuu yao ya Morocco.

Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake Disemba mwaka 2021 kutokana na kuidai klabu hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili (signing fee).

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA UBINGWA WA LIGI NA ASFC...NABI KAAMUA 'KUWAPA MAKAVU LIVE' MASTAA WAKE...