Home Uncategorized OLE GUNNAR JICHO LAKE KWA NAHODHA WA ASTON VILLA

OLE GUNNAR JICHO LAKE KWA NAHODHA WA ASTON VILLA


 JICHO la Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskajer linatajwa kuvutiwa na uwezo wa nyota wa Klabu ya Aston Villa, Jack Grealish ambaye amezidi kuwa bora ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu England.

Usiku wa kuamkia leo Manchester United ilishinda mabao 2-1 Uwanja wa wa Old Trafford dhidi ya Aston Villa na kusepa na pointi tatu mazima zinazowafanya wafikishe jumla ya pointi 33 sawa na mabingwa watetezi Liverpool ambao wapo nafasi ya kwanza kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungana.

Mabao ya United yalifungwa na Antony Martial dakika ya 40 na lile la ushindi lilifungwa na Bruno Fernadez dakika ya 61 kwa penalti huku bao la Aston Villa likifungwa na Bertrand Traore dakika ya 58.

Tangu msimu uliopita United ilikuwa inahitaji saini ya nyota huyo ambaye ni nahodha ambapo Ole anatajwa kuuliza bei ya mchezaji huyo ili aweze kumvuta ndani ya Old Trafford.

Nyota huyo amesaini dili la miaka mitano kuendelea kutumika ndani ya kikosi hicho baada ya kusaini dili hilo Septemba kilichowashinda United ni dau lake ambalo walitajiwa kuwa ni Euro milioni 100 jambo lililowarudisha nyuma.

SOMA NA HII  BEKI SIMBA ASAINI YANGA