Home Uncategorized ISHU YA JUMA ABDUL KUREJEA YANGA IPO HIVI

ISHU YA JUMA ABDUL KUREJEA YANGA IPO HIVI


JUMA Abdul, beki wa zamani wa Klabu ya Yanga amesema kwa sasa anafikiria zaidi kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na kuna dili analisubiri na kama likitiki tu anasepa.

 

Beki huyo mtaalamu kwa krosi amesema kwa sasa hajasaini timu yoyote hapa nchini labda dili lake la kwenda nje likwame ndipo anaweza kufikiria timu nyingine ya kwenda.


Akiwa Yanga msimu wa 2019/20 alitoa jumla ya pasi sita za mabao kwa mguu wake wa kulia aliachwa na Yanga baada ya kushindwana kwenye masuala ya mkataba.

 

Abdul pamoja na beki mwingine wa kati, Kelvin Yondani walitangazwa kuachwa na Yanga klabu ambayo waliitumikia kwa miaka nane. Ilidaiwa Yanga iliachana na wachezaji hao kwa madai ya kushindwana katika maslahi.

 

Hata hivyo kumeibuka maneno kuwa klabu hiyo imepanga kuwaita tena mezani wachezaji hao wazoefu ili kufanya nao mazungumzo ya kuwemo katika kikosi hicho msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  HILO DAU LA LEROY SANE WA MANCHESTER CITY LAZIMA UKAE