Home Uncategorized TOTTENHAM WANAHAHA KUMPATA DYBALA

TOTTENHAM WANAHAHA KUMPATA DYBALA


TOTTENHAM wapo bize kwa sasa kukamilisha dili la kumpata mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala.

Kwa sasa wamefikia hatua nzuri ya makubaliano na uongozi wa Juventus kuhusu kumpata nyota huyo.

Mpango mkubwa wa Dybala ni kutimka ndani ya Juve ili kupata changamoto mpya Jambo lililoongeza wepesi kwa Spurs kumkomalia.

Nyota huyo hayupo tayari kutua Manchester United kwa dau dogo licha ya klabu yake kufika makubaliano ya mwisho na mabosi wa United.

Tottenham wapo tayari kukidhi matakwa ya mshambuliaji huyo kwa kumlipa angalau pauni 300 kwa wiki.

United wao walipendekeza dili la kubadilishana na mchezaji Romelu Lukaku ila liliyeyuka kabla ya kukamilika

SOMA NA HII  MAMBO BADO SIO SHWARI LAKINI LAZIMA KUJIPANGA NA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA