Home Uncategorized YANGA: HAKUNA TIMU YENYE REKODI YA KUJAZA UWANJA WA TAIFA KIMATAIFA KAMA...

YANGA: HAKUNA TIMU YENYE REKODI YA KUJAZA UWANJA WA TAIFA KIMATAIFA KAMA SISI


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hakuna rekodi ambayo imewahi kuvunjwa na timu yoyote ya kujaza uwanja wa Taifa mapema tangu walipofanya wao Julai 28 mwaka 2016 kwenye michuano ya kimataifa ambapo Yanga ilicheza na TP Mazembe.

Yanga imesema kuwa kwenye mchezo huo mapema saa 6 mchana walikuwa wamejaza uwanja huo na mageti yote kufungwa ili kuzuia mashabiki waliokuwa nje wasiingie ndani.

Barabara zote zilijaa wananchi na ilibidi zifungwe na Polisi walitumika kuzuia wananchi wasiingie ndani ya uwanja na kuwatuliza wale waliokuwa nje.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kwa sasa mashabiki wanatakiwa wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa siku ya jumamosi kushuhudia ushindani kati yao na wapinzani wao Township Rollers uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  KOCHA MKUU WA SIMBA ATAJA KITAKACHOMREJESHA MLIPILI KIKOSI CHA KWANZA