Home Azam FC AZAM FC YAMALIZANA NA MSHAMBULIAJI WA ZAMBIA

AZAM FC YAMALIZANA NA MSHAMBULIAJI WA ZAMBIA


MABOSI wa Dar, Klabu ya Azam FC imemtambulisha nyota mpya leo Julai 19 kwa mashabiki wao.

Ni mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa usajili huru akitokea Zanaco ya huko Zambia.


Taarifa iliyotolewa na Azam FC imeeleza kuwa mshambuliaji huyo mzoefu, mrefu na mwenye umbo kubwa, amesaini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya kudumu ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2023.

Kola anakuja kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya ushambuliaji, kuanzia msimu ujao 2021/2022.

Aidha Kola ambaye wakala wake ni Nir Karin, akiwa Zanaco msimu uliopita, alifunga jumla ya mabao 14 katika mashindano mbalimbali nchini Zambia.

SOMA NA HII  KIMENUKA CHAMAZI.... KISA KUMTUSI MENEJA.... AZAM FC KUWAFUKUZA AGGREY MORRIS, 'SURE BOY'..