Home news MAUZO YA JEZI ZA SIMBA YAVUNJA REKODI BONGO…KWA SIKU MBILI YAINGIZA BILIONI...

MAUZO YA JEZI ZA SIMBA YAVUNJA REKODI BONGO…KWA SIKU MBILI YAINGIZA BILIONI 3.15


Katika hali isiyo ya kawaida, mashabiki wa Simba SC wamezigombania jezi mpya  za msimu huu ambapo ndani ya saa 48 zaidi ya jezi pisi  zimeuzwa 90,000

Akithibitisha taarifa hizo, Afisa Masoko wa Vunja Bei Fadhili Ngajilo, ambao ndio wauzaji wakuu wa jezi za Simba Msimu huu, amesema kuwa hadi jana jezi za Polo zilikuwa zimesha kabisa.

Aidha, Fadhili amesema kuwa pia wamemaliza jezi za jumla , hivyo kwa wanaotaka kununua jezi kwa jumla wafike kwenye maduka yao wiki ijayo.

Hii inakuwa ni rekodi ya kwanza kuwekwa katika soka la Tanzania, ambapo inawaacha mbali watani zao Yanga SC ambao wao mpaka siku ya tamasha lao la Siku ya Wananchi juzi, inasemekana walikuwa wameuza jezi pisi 30,000.

SOMA NA HII  PAMOJA NA UJIO WA KOCHA MPYA..UBOVU WA SIMBA HUU HAPA...USAJILI NA SAKATA LA MO DEWJI VYATAJWA..