Home Habari za michezo UNAIKUMBUKA ILE ‘MOMENTI’ YA AZIZ KI KUSHANGILIA NA MAKAMBO JUZI…BASI KUMBE NYUMA...

UNAIKUMBUKA ILE ‘MOMENTI’ YA AZIZ KI KUSHANGILIA NA MAKAMBO JUZI…BASI KUMBE NYUMA YA PAZIA KUNA HILI KATI YAO…


SABABU kubwa ya Aziz KI kumfuata Heritier Makambo baada ya kufunga bao mbele ya Mtibwa Sugar ni ahadi ambayo alipewa.

Mtu wa karibu wa wachezaji hao amesema kuwa Makambo alimuamuambia Aziz KI kuwa atafanya jambo lolote kwenye mchezo huo kufunga ama kutoa pasi.

“Makambo alipokuwa benchi alimuambia Aziz KI nenda uwanjani una bao lako hapo kama sio bao itakuwa ni asisti,” .

Aziz KI alifunga bao lake la kwanza kwenye ligi mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikishinda mabao 3-0.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa bado kazi ipo kwa ajili ya mechi zijazo kwenye ligi na kimataifa.

SOMA NA HII  MFAHAMU ZAIDI STRAIKA MPYA MZUNGU WA SIMBA ALIYEPELEKEA KAGERE NA MUGALU KUTEMWA ...