Home news BAADA YA KUONA WENZAKE WALIVYOCHEZA DHIDI YA SIMBA…YACOUBA AIBUKA NA HILI ..ATUPA...

BAADA YA KUONA WENZAKE WALIVYOCHEZA DHIDI YA SIMBA…YACOUBA AIBUKA NA HILI ..ATUPA DONGO…


BAADA ya ngoma ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga kumalizika kwa suluhu, nyota wa Yanga, Yacouba Songne aliwataja mabeki wa Simba, Henock Inonga na Joash Onyango kuwa chanzo cha matokeo yale.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yacouba alikuwa jukwaani akishuhudia mechi bila kuwa sehemu ya mchezo kutokana na kuuguza majeraha ya goti.

Baada ya mechi kumalizika bila bao, Gazeti la Mwanaspoti lilipiga stori na Yacouba ambaye aliuchambua mchezo kwa ujumla na kuwataja Inonga na Onyango.

“Ilikuwa mechi bora kwa pande zote mbili, Yanga ilicheza mpira wake wa kila siku, ilimiliki mpira katika vipindi vyote lakini ilishindwa kufunga kutokana na safu ya ulinzi ya Simba kuwa imara,” alisema Yacouba na kuongeza;

Mabeki wa kati wa Simba, Inonga na Onyango walicheza vizuri sana, walikuwa wakisambaratisha kila mipango ya Yanga na mechi kuisha kwa sare, alisema Yacouba ambaye ni raia wa Burkina Faso.

Yacouba alizungumzia pia majeraha yake na kufunguka kuwa siku si nyingi atarejea uwanjani.

“Nilitamani kuwepo kwenye mechi hii lakini ndio hivyo nina majeraha, nashukuru matibabu yalifanyika vizuri na sasa naendelea vizuri chini ya uangalizi wa daktari, siku si nyingi nitarejea.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA...HUU HAPA MSIMAMO WA SIMBA KUENDELEA NA MGUNDA...