Home news RASMI…SIMBA KUFYEKA WATANO DIRISHA DOGO…WAWA, BOCCO NA NYONI WATAJWA…BARBARA AFUNGUKA..

RASMI…SIMBA KUFYEKA WATANO DIRISHA DOGO…WAWA, BOCCO NA NYONI WATAJWA…BARBARA AFUNGUKA..


SIMBA huenda ikaachana na wachezaji watano mwishoni mwa msimu huu mara baada ya mikataba yao kumalizika, kati ya hao yupo beki Muivory Coast, Pascal Serge Wawa.

Hiyo ni katika kuhakikisha wanakuwa na kikosi imara kitakachofanya vizuri msimu ujao kwenye mashindano mbalimbali. Tayari uongozi wa Simba umeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wapyawatakaowasajili.

Mmoja wa mabosi wa Simba, ameliambia amesema kuwa,  wachezaji hao baadhi wataachwa kutokana na umri mkubwa walionao.

Bosi huyo alisema wachezaji hao wamekosa kasi, hivyo Kocha Mkuu, Pablo Franco amependekeza wachezaji hao ambao majina yao yamefichwa kwa sasa.

Aliongeza kuwa, tayari majina hayo kocha ameyakabidhi kwa uongozi, hivyo mwishoni mwa msimu watatangazwa.

“Zaidi ya wachezaji watano huenda Simba wakaachana nao mwishoni mwa msimu, kati ya hao yupo Wawa.

“Kwa sasa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, nafasi yake imechukuliwa na Inonga (Hennock) ambaye anacheza kwa kuelewana na Onyango (Joash).

“Wachezaji wengine wanaotajwa ni wale ambao umri umekwenda na hawapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza,” alisema bosi huyo.

Miongoni mwa wachezaji wenye umri mkubwa ni pamoja na John Bocco, Erasto Nyoni, Meddie Kagere na Mzamiru Yassin

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, hivi karibuni alizungumzia usajili kwa kusema: “Tumepanga kufanya maamuzi magumu katika usajili wetu kwa kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa watakaofanya vema katika mashindano ya kimataifa.”

SOMA NA HII  NYOTA SABA KIKOSI CHA KWANZA KUUZWA NA MANCHESTER UNITED