Home Habari za michezo MZEE WA KUWAJAZA ANUKIA COASTAL UNION…YANGA SC WAANIKA DILI LILILOKATALIWA…

MZEE WA KUWAJAZA ANUKIA COASTAL UNION…YANGA SC WAANIKA DILI LILILOKATALIWA…

Staa wa Yanga SC Makambo atakiwa na Coastal Union

UONGOZI wa Coastal Union umetuma maombi ya kuhitaji saini ya straika wa Yanga SC, Yusuf Athuman na Heritier Makambo ili kuitumikia timu hiyo kwa miezi sita.

Wagosi wanataka kufanya usajili katika dirisha dogo ili kuhakikisha inafanya vizuri na kuendelea kusalia Ligi Kuu msimu ujao.

Mmoja wa vigogo wa timu hiyo, alisema kuwa wametuma maombi ya kuwaomba kwa mkopo Athuman na Makambo ili kuongeza nguvu kwenye eneo hilo.

β€œTumeona watatufaa, tunasubiri majibu yao, ila sisi tunahitaji huduma zao,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa msemaji wa Yanga SC, Ally Kamwe alisema kwa kifupi; ”Ni kweli hilo lipo, ila Yusuph hajakubali na Makambo timu nyingi zinamtaka.”

Yusuf Athuman aliyesajiliwa kutoka Biashara United kwa msimu huu hajacheza mchezo wowote wa Ligi Kuu lakini, amefunga mabao mawili katika michuano ya ASFC walipoifumua Kurugenzi Simiyu kwa mabao 8-0.

Kwa upande wa Makambo naye hajapata nafasi kikosi cha kwanza bado hajawa kwenye fomu na anahitaji kwenda sehemu ambayo atapata muda mwingi wa kucheza.

SOMA NA HII  YANGA SASA AKILI YOTE KWASIMBA, MAANDALIZI YAKE SIO POA