Home Habari za michezo UONGOZI WA SIMBA WAMPA NENO HILI SAMIA BAADA YA MAREKEBISHO YA UWANJA...

UONGOZI WA SIMBA WAMPA NENO HILI SAMIA BAADA YA MAREKEBISHO YA UWANJA WA MKAPA

Habari za Simba

Uongozi wa Klabu ya Simba SC, umeipongeza serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya marekebisho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa wakati kuweza kuutumia katika ufunguzi wa michuano ya African Football League dhidi ya AI Ahly.

Februari 22 mwaka huu Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), ilishauri uwanja huo kufungwa na kutotumika kwa muda ili kupisha ukarabati.

Simba SC itakuwa wenyeji wa Al Ahly ya Misri katika mchezo huo wa ufunguzi utakaochezwa Oktoba 20, mwaka huu katika uwanja huo.

Akizungumza Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa jezi maalum zitakazotumika katika michuano hiyo, Mwenyeketi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Salim Abdalah ‘Try Again’ amesema anaipongeza serikali kwa kuhakikisha ůwanja unakarabatiwa kwa wakati na utaanza kutumika katika ufunguzi wa michuano hiyo

Amesema kwa upendo ulioonyeshwa na serikali, Simba watahakikisha wanapambana kufanya vizuri katika mchezo huo.

“Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama tusipoipongeza serikali chini ya Rais Dk Samia kwa a kuhakikisha uwanja unakarabatiwa kwa haraka ili tuweze kushiriki michuano hii muhimu na ya kipekee,” amesema Try Again.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu amesema wameweka historia mpya ya kuzindua jezi maalum kwa ajili ya michuano hiyo muhimu.

“Baada ya uzinduzi wa jezi hizi kwa ajili ya michuano hii zitaweza kupatikanä katika kila duka, hivyo tunahitajl kuona mashabiki na wapenzi wa Simnba wanazinunua kwa wingi,” amesema.

Michano hiyo itashirikisha timu nane ambazo ni Simba, A Ahly (Misri), TP Mazenbe (DRC) Esperance (Tunisia) Enyimba (Nigeria) Wydad Casablanca (Morocco) Petro Atletico (Angola) na Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini).

SOMA NA HII  MWENYEKITI WA SIMBA AUAWA NA WATU WASIO JULIKANA