Home Uncategorized UEFA YASIMAMISHWA MPAKA 2021

UEFA YASIMAMISHWA MPAKA 2021

UEFA imesitisha michuano hiyo ndani ya mwaka huu 2020 mpaka 2021 kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Kutokana na kuenea kwa Virusi vya Corona ambavyo vilianza kusambaa mwezi Januari, wamesitisha michuano hiyo na inatarajiwa kuanza kufanyika 2021 kati ya Juni 11 mpaka Julai 11 mwaka ujao.

Kutokana na kikao cha leo, Machi 17, Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin ameamua kusimamisha msimu huu michuano hiyo mpaka msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa Leo na UEFA imeeleza kuwa :” UEFA leo inatangaza kusitisha michuano ya UEFA Euro 2020 kutokana na thamani ya afya za wachezaji na mashabiki kuwa bora kuliko jambo lolote na mpango wetu ni kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima hii ni kutokana na kusambaa kwa kasi Virusi vya Corona.


 “Mechi zote za UEFA na mechi za kirafiki kwa klabu na timu za Taifa kwa Wanawake na Wanaume zinasitishwa mpaka pale tutakapotoa taarifa, mechi zilizotarajiwa kuchezwa mwezi Machi sasa zinaweza kuanza mwezi Juni lakini itategemea na hali itakavyokuwa,’.

SOMA NA HII  YANGA HALI TETE LIGI YA MABINGWA ALLY KAMWE ATOA KAULI TATA