Home Uncategorized ISHU YA LIGI KUSIMAMISHWA SIMBA WAIGUSIA, WAICHOKONOA KIANIA KLABU NYINGINE

ISHU YA LIGI KUSIMAMISHWA SIMBA WAIGUSIA, WAICHOKONOA KIANIA KLABU NYINGINE


HAJI Manara amesema kuwa masha ya Watanzania ni muhimu kuliko mpira lakini ana imani kwamba utaratibu upo wazi.

Serikali imesimamisha masuala yote ya michezo kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kupambana na ugonjwa wa Corona na kwenye Ligi Kuu Bara hakuna bingwa isipokuwa Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71.

Manara ameandika hivi kwenye Ukurasa wake wa Instagram:”Kuna klabu inaombea ligi isimamishwe,Yes afya na maisha ya Wabongo ni Muhimu zaidi kuliko mpira lakini Utaratibu upo wazi.

“Bingwa wa msimu uliopita ataendelea na uchampioni wake au anaeongoza ligi atapewa haki yake,” .

SOMA NA HII  AZAM MEDIA YABORESHA HUDUMA,YAZINDUA KISIMBUSI CHA DIGITAL