Home Uncategorized YANGA WAFAFANUA ISHU YA MCHEZAJI WAO MORRISON KUTOCHEZA SIMBA

YANGA WAFAFANUA ISHU YA MCHEZAJI WAO MORRISON KUTOCHEZA SIMBA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hauna taarifa kuhusu nyota wao wa zamani Bernard Morrison kufungiwa kucheza kutokana na kesi yake inayohusu mkataba wake.

Morrison baada ya kujiunga na Simba akitokea Klabu ya Yanga, mabosi wa timu hiyo waliweka wazi kuwa wamepeleka kesi hiyo kuhusu utata wa mkataba wake kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya masuala ya Michezo,(Cas).

Hatua hiyo ilifikia huko baada ya kesi yake ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuhusu mkataba wa mchezaji huyo ambayo ilisikilizwa kwa muda wa siku tatu kueleza kuwa kulikuwa na utata kwenye mkataba wake.

Baada ya TFF kutoa tamko hilo waliwapa nakala ya kesi mabosi wake wa zamani Yanga na Simba huku wakisema kuwa mchezaji huyo atakuwa huru kujiunga na timu anayohitaji.

Morrison aliamua kujiunga na Simba ambapo alisaini dili la miaka miwili kuwatumikia mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Fredric Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa anachotambua kuhusu suala la mchezaji huyo ni kwamba ana kesi ya kujibu ila kuhusu kuzuiwa kucheza hajapata taarifa hizo.

“Ninachojua mimi kuhusu Morrison ni kwamba yeye yupo na kesi ya kujibu kuhusu mkataba wake na hizo ni taarifa ambazo ni rasmi kutoka Cas.

“Kuhusu kufungiwa kucheza mpira ndani ya uwanja hilo mimi sijui kwa sababu haijawa rasmi na sina taarifa zake kuhusu hilo.

“Hakuna barua ambazo nimepata ila kwa kuwa ni kesi huwezi kuweka kila kitu wazi kwa sasa, kikubwa mashabiki wawe na subira na kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

Morrison ndani ya Simba amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza kwa sasa kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa na viongozi wa Simba kwamba anaumwa.

Kwenye Kombe la Mapinduzi, visiwani Zanzibar kiungo huyo alipata nafasi ya kupasha muda mfupi kabla ya dakika 90 kukamilika ila hakuingia kwenye fainali dhidi ya mabosi wake wa zamani Yanga.

SOMA NA HII  RUVU SHOOTING WAPANIA KUENDELEA KUGAWA DOZI KAMA KAWAIDA