Home Uncategorized BOSI WA SIMBA AFUNGUKIA MAISHA YAKE NDANI YA YANGA

BOSI WA SIMBA AFUNGUKIA MAISHA YAKE NDANI YA YANGA



SENZO Mbatha, mshauri mkuu ndani ya Klabu ya Yanga kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko amesema kuwa anafurahia maisha yake ya sasa ndani ya timu hiyo kutokana na sapoti anayopata.


Mbatha aliibukia ndani ya Yanga akitokea Klabu ya Simba muda mfupi baada ya kutangaza kujiuzulu nafasi yake ambapo alikuwa ni bosi ndani ya Simba akiwa ni Mtendaji Mkuu,(C.E.O).

Mbatha amesema:-“Ninaheshimu kuhusu Yanga kwa kuwa ina namba kubwa ya mashabiki, namba kubwa ya wadhamini ambao wapo ndani yake ikiwa ni pamoja na Kampuni ya GSM, wadhamini wetu SportPesa.


“Ninafurahia kufanya kazi na mwenyekiti Msolla,(Mshindo) sapoti ambayo tunapata inatupa matokeo mazuri ya kile ambacho tunakihitaji hasa kwa sasa tukiwa kwenye aina ya mpira wa kisasa.

“Mpira wa kisasa unahitaji kila kitu kuwa bora kuanzia sehemu ya kuchezea sehemu ya mazoezi, miundombinu pamoja na ushirikiano jambo ambalo linatupa nguvu.

“Katika kila jambo tunajiandaa kwa utayari ili kuweza kuleta ushindani ndani na nje ya uwanja,” amesema.

Akiwa kiongozi ndani ya Yanga, ameshuhudia timu yake ikicheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara ambapo ilikuwa ni mbele ya Tanzania Prisons kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na mchezo wa pili ilikuwa mbele ya Mbeya City, ilishinda bao 1-0 zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa.
SOMA NA HII  YANGA NOMA, YAMALIZANA NA MAJEMBE TISA FASTA, LISTI YAO KAMILI HII HAPA