Home Uncategorized CHAMPIONI NA SPOTIXTRA ZATINGA MTAANI KUPAMBANA NA CORONA

CHAMPIONI NA SPOTIXTRA ZATINGA MTAANI KUPAMBANA NA CORONA

GLOBAL Publishers kupitia magazeti yake ya michezo ya Championi na Spoti Xtra, imeanzisha kampeni ya kuzuia kusambaa kwa Virusi vya Corona na kuvitokomeza kabisa.

Katika kampeni hiyo, timu ya Global Publishers ilitembelea mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kuweka ndoo maalum za maji ambapo watu watakuwa wakinawa katika kujikinga na Corona.

Baadhi ya mitaa ambayo timu ya Global Publishers ilitembelea ni kituo cha daladala cha Makumbusho na Simu 2000 maarufu kama Mawasiliano.


Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo amesema:-“Tumeamua kujitolea kuisadia jamii na serikali kwa jumla kupambana na ugonjwa wa Covid-19. 

” Sisi ni sehemu ya jamii, tunajua umuhimu wa afya za wasomaji wetu, afya za wanamichezo na Watanzania kwa jumla. Tuendelee kujikinga kwa kuwa ugonjwa wa Covid-19 si jambo la utani,” .

SOMA NA HII  JESHI LA DODOMA FC LEO DHIDI YA YANGA,SHEIKH AMRI ABEID