Home Uncategorized UJUMBE HUU WA ALLIANCE WATUMWA YANGA

UJUMBE HUU WA ALLIANCE WATUMWA YANGA

Habari za Michezo leo

FELIX Minziro, Kocha Mkuu wa Alliance amesema kuwa wanatambua wana kazi ngumu ya kufanya leo mbele ya Yanga ila wapo tayari hawana hofu.

Alliance itakaribishwa na Yanga Uwanja wa Taifa majira ya saa 11:00 jioni ikiwa ni mchezo wa pili kukutana msimu huu kwenye ligi.

Minziro amesema: “Tunawatambua wapinzani wetu hatuna hofu nao kwani wachezaji wapo sawa nasi tutapambana kupata pointi tatu muhimu,”.

Mchezo wa kwanza Alliance ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

SOMA NA HII  TFF YA BOTSWANA YAIRAHISHIA KAZI YANGA